Kiatu kilichofunga bao
katika fainali ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kimeuzwa kwa uero milioni
2 (Sh bilioni 4.2).
Kiatu hicho ni mali ya
mshambuliaji wa Ujerumani, Mario Gotze ambaye alifunga bao hilo pekee na
kuiangusha Argentina kwa bao 1-0.
Kiatu hicho kiliingizwa
kwenye mnada maalum, kiuzwe na fedha zake zitumike kusaidia watoto wenye
matatizo.
Gotze ambaye hakuwahi
kukisafisha kiatu hicho tokea fainali, alikubali fedha ziwasaidie watoto
kupitia mradi wa 'A Heart for Children', lakini hakuna aliyejua kitafikia bei hiyo.
Hali hiyo imeonyesha
kuwashangaza wengi lakini imezidi kuonyesha kiasi gani mpira una nguvu.










0 COMMENTS:
Post a Comment