KATIBU MKUU MPYA WA YANGA, DK TIBOROHA AKIZUNGUMZA NA KOCHA MSAIDIZI, CHARLES BONIFACE MKWASA NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA TFF ALIYEWAHI KUWA MENEJA WA YANGA, AYOUB NYENZI. |
Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha
ameonyesha tofauti kubwa ya kwamba suala la rangi si ishu.
Kwa mara ya kwanza alipohudhuria mazoezi ya
Yanga baada ya kutangazwa kuchukua nafasi ya Beno Njovu, Dk Tiboroha alikuwa
amevaa shati la rangi nyekundu iliyokosa kama damu yam zee.
Dk Tiboroha alitinga mazoezini Yanga na
kutambulishwa kwa Kocha Hans van der Pluijm na benchi zima la ufundi.
Kiongozi huyo ambaye amewahi kusoma na
kufanya kazi katika nchi za Sweden na Denmark, ameonyesha kukataa ule utamaduni
wa kiongozi wa Yanga kuonekana kama amekosea iwapo atavaa nguo za rangi
nyekundu.
Msemo wa SALEHJEMBE: “Si kila njano ni Yanga
au kila nyekundu ni Simba.”
Ila huenda daktari huyo wa michezo akashawishiwa kuachana na rangi ya 'Simba', tusubiri.
0 COMMENTS:
Post a Comment