| KESSY. |
Beki wa kulia wa Mtibwa
Sugar, Hamis Kessy, amefunguka kuwa baada ya kuwatajia dau la shilingi milioni
35, Simba, ambayo inamuwania kumsajili, viongozi wa kikosi hicho wala
hawajarudi tena kuzungumza naye.
Simba ina uhaba wa beki ambapo
haikufanya vizuri katika mechi saba za mwanzo na kujikuta ikitoka sare mechi
sita na ikishinda moja tu.
Kessy amesema kuwa, kuna
viongozi wa Klabu ya Simba ambao walimfuata wakitaka kumsajili kwa ajili ya
kuichezea timu hiyo msimu ujao lakini amewapa sharti la kuhakikisha wanampa milioni
35 na kama itashindikana basi hatakubali kuondoka katika klabu yake hiyo ya
sasa.
“Mimi nilifuatwa na Makamu
Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kutaka kunisajili na nikawataarifu
kuwa dau langu ninalolihitaji ni shilingi milioni 35, hivyo hawajarudi
kuzungumza na mimi tena.
“Kuhusu upande wa viongozi
wenyewe wameniruhusu kwani walikuwa wakisubiri majibu yangu na kuona kama
nimeridhika kuondoka na wala hawana tatizo na wanachotaka wao ni taratibu
kufuatwa,” alisema Kessy.







0 COMMENTS:
Post a Comment