Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema wanafanya usajili
kwa umakini kurekebisha kikosi, lakini akasisitiza waamuzi lazima wachezeshe
kwa haki.
Hans
Poppe akaenda mbali zaidi kwa kusema katika mechi saba za Ligi Kuu Bara,
waamuzi walichemsha huku akitolea mfano wa bao moja la kiungo wa Yanga, Simon
Msuva kwamba alipewa tu na mwamuzi.
Hans Poppe alisema katika mechi ya Yanga ilipokuwa
ikiivaa Mgambo JKT na Msuva kufunga mawili, moja halikuwa halali.
“Tunaweza
kusajili timu nzuri, lakini kama waamuzi hawatakuwa ‘fair’, basi ni kazi bure.
Nawaasa wawe fair ili kila timu ishinde kwa uwezo wake na ndiyo maana ya
kusajili timu bora.
“Katika
mechi kadhaa niliona Simba tukibaniwa makusudi, mfano mechi yetu na Yanga. Kwa
makusudi mwamuzi alimuachia yule Jaja, akabaki na kipa lakini akapaisha.
“Lakini
niliona mechi ya Yanga dhidi ya Mgambo, nilikuwa naangalia kwenye runinga.
Ajabu kabisa bao alilofunga yule kijana Msuva halikuwa halali.
“Kabla
hajafunga, kipa wa Mgambo alivamiwa na watu wawili, kila mmoja aliona, mwamuzi
akamuacha Msuva afunge.
“Bao
jingine la Msuva siku hiyo, sina shida nalo. Watu walisema aliotea lakini mimi
niliona lilikuwa ni clean goal (bao safi),” alisema Hans Poppe na kuongeza.
“Mechi
yetu na Coastal, hadi wanakwenda kupata faulo ya bao la pili, mwamuzi
aliashiria vitendo tofauti, watu wakasimama.
“Lengo
si kumsema mtu au vipi, hii ni mifano michache. Ninashauri waamuzi wabadilike,
waachane na mambo ya kukiuka sheria na hii inapunguza morali na ushindani wa
ligi.”
Hans
Poppe alisisitiza Simba inaendelea kumalizia usajili katika sehemu kadhaa kwa
ajili ya kujiimarisha zaidi ili kumaliza msimu ikiwa sawasawa.







Tayari Hanspope kashachanganyikiwa maana taarifa ya kufungwa goli 4 siku ya mtani jembe anazo!
ReplyDelete