December 14, 2014

KIKOSI CHA SIMBA KATIKA MECHI YA NANI MTANI JEMBE. KILIANZA NA WAGANDA WATATU. SSERUNKUMA, MURISHID NA OKWI.

Ile rekodi ambayo SALEHJEMBE ilieleza kwamba Simba inakaribia kuifikia ya kuwa na wachezaji watano wa kigeni kutoka taifa moja, imetimia.

Simba sasa ina wachezaji watano wa kigeni kutoka nchi jirani ya Uganda.
Hali hiyo inatokana na kutemwa kwa mfungaji bora msimu uliopita, Amissi Tambwe na kiungo Pierre Kwizera raia wa Burundi.

Simba imewaacha Warundi hao na kuwasajili kiungo Simon Serunkuma na Juuko Murishid ambao wamecheza mechi dhidi ya Yanga jana, wakaivutia kamati ya usajili.

Maana yake Simba itakuwa na wachezaji wote kutoka Uganda ambao ukiachana na hao wawili, kuna Danny Sserunkuma ambaye pia ni mpya halafu Emmanuel Okwi na Joseph Owino, wote kutoka Uganda.

Wachezaji wa kimataifa ambao wameichezea Simba muda mwingi huku wakiondoka na kurudi zaidi ya mara moja ni Owino na Okwi.

Wawili hao walijiunga na Simba miaka sita iliyopita, Okwi akitokea Villa na Owino URA.

Baadaye Okwi aliondoka na kujiunga na Etoile du Sahel ambako aliuzwa bure na Simba chini ya Ismail Aden Rage, kabla ya kujiunga na AS Villa, Yanga na baadaye akarudi Simba.

Owino yeye alirejea kwao Uganda, baadaye akarudi nchini na kujiunga na Simba kabla ya kujiunga na Simba kwa mara nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic