![]() |
| KESSY (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA TSHABALALA WA SIMBA. |
Uongozi wa Klabu ya Simba umefunguka kuwa, upo
katika hatua za mwisho za kumalizana na beki namba mbili wa Mtibwa Sugar, Hamis
Kessy licha ya kuripotiwa kuwepo kwa ugumu wa mchakato huo wa usajili.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba mazungumzo yako katika hatua nzuri sana na pande zote mbili, yaani Simba na Mtibwa Sugar zimekubali kwamba zimefanya mazungumzo.
Simba ambayo imeshampa mkapata wa miaka mwili
raia huyo wa Uganda, imekuwa katika mazungumzo ya kumsajili Kessy licha ya kuwa
Mtibwa imekuwa ikiweka ngumu, kuna uwezekano wa kukubali kutokana na mchezaji
mwenyewe kuonyesha nia ya kukubali dili.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alifunguka kuwa mazungumzo
yanaendelea vizuri na kama kila kitu kitaenda vizuri, kuna uwezekano wa usajili
huo kukamilika ndani ya siku chache zijazo.
“Tupo katika mazungumzo ya mwisho na mchezaji
wa Mtibwa, Kessy ambapo wakati wowote kuanzia sasa tutamalizana naye kwa
kuingia mkataba mara baada ya kufikia makubaliano na uongozi wake,” alisema
Hans Poppe.
Mkurugenzi
wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser, alisema ni kweli mazungumzo yanaendelea.
“Tumezungumza na Simba, lakini bado
hatujakubaliana, nia yetu haikuwa kumuuza mchezaji yeyote kwa sasa lakini
inavyoonekana hata yeye mwenyewe (Kessy), ameonyesha nia ya kutaka kwenda
Simba, hivyo tutakujulisha nini kinachoendelea,” alisema kiongozi huyo.
Wakati huohuo, mchakato wa Simba kumuwania beki
mwingine wa timu hiyo, Salim Mbonde, umeendelea lakini dalili zinaonyesha kuwa
Mtibwa imegoma katakata kumuuza mchezaji huyo.
Taarifa kutoka Mtibwa
zinaeleza kuwa klabu hiyo inahofia kuuza wachezaji wake muhimu kwa kuwa ligi
bado inaendelea, hivyo suala la kumuuza mchezaji huyo kwa sasa wamelifuta
rasmi.








0 COMMENTS:
Post a Comment