Uongozi wa Simba umechukua uamuzi wa kusitisha
kumsajili mshambuliaji Danny Mrwanda wa Polisi Morogoro.
Simba imefikia uamuzi huo baada ya kugundua
hakusema ukweli kuhusiana na mkataba wake na Polisi Morogoro.
Habari za uhakika zimeeleza, Mrwanda hakuiambia
Simba kama mkataba wake unamzuia kusaini hapa nchini lakini unamruhusu kwenda
nje ya Tanzania bila ya kipingamizi.
“Polisi Moro walipiga simu Simba kuwauliza
malipo yao, hiyo ikawashitua kwa kuwa walikuwa hawajasaini na Mrwanda
hakuwaambia kama Polisi wanatakiwa kulipwa,” kilieleza chanzo.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe, alithibitisha hilo kwa kusema: “Tumemwambia
akazungumze na uongozi wa Polisi, wamalizane na kumpa barua ya kumruhusu.
“Ikiwa hivyo tutamsainisha, isipokuwa hivyo,
basi tutafanyaje. Maana hakutuambia vizuri mwanzo kuhusu hilo.”








0 COMMENTS:
Post a Comment