December 29, 2014


Straika wa zamani wa Simba, Mrundi Amissi Tambwe, amemtetea mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Mganda Danny Sserunkuma, kuwa atawika sana kwenye klabu hiyo.


Tambwe ambaye amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Simba amefikia hatua hiyo baada ya mashabiki wa timu huyo kuanza kumtupia lawama kuwa hana lolote kutokana na kiwango cha chini alichokionyesha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba ilitandikwa bao 1-0 huku Sserunkuma akionyesha kiwango kibovu.

Tambwe amesema Simba wasikate tamaa kwani kufanya hivyo ni mapema mno.

”Sserunkuma siyo mchezaji mbaya ni mchezaji mzuri sana ila tu Simba wanatakiwa kumpa muda na wasianze kumkatisha tamaa mapema akashindwa kucheza.


“Naamini kabisa wakiwa wavumilivu atawasaidia kwa sababu ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki Kati,” alisema Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic