AME ALI |
Straika wa Mtibwa Sugar, Ame Ali ‘Zungu’,
amesema lazima ‘pachimbike’ pale atakapokutana na beki wa Ruvu Shooting George
Michael, aliyemfanyia ‘umafia’ mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe kwenye mchezo
wa ligi kuu kati ya Yanga na Ruvu Shooting wiki iliyopita.
Ruvu Shooting ambao wanashika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 12, kesho Jumapili watashuka kwenye Uwanja wa Mabatini kuvaana na Mtibwa inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 17.
Mshambuliaji
huyo ambaye anashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ufungaji akiwa na mabao 5
nyuma ya Didier Kavumbagu mwenye mabao 7, alisema licha ya beki huyo kuwa gumzo
kwa sasa, yeye hatishiki hata kidogo kukutana naye.
Alisema kuwa haamini kama kuna beki hatari
ambaye ataweza kumzuia asifanye mambo yake uwanjani kwani ameshakutana na
mabeki ambao walikuwa wakiaminika kuwa ni wakali lakini walichemsha kumkaba.
“Kwa sasa naangalia kuongeza mabao ili niwe
mfungaji bora, hivyo nimejiandaa kikamilifu na hivyo hata kidogo simuogopi na
hawezi kunizuia kufanya yangu, kwanza siamini kama kuna beki anayeitwa kisiki
ambaye ataweza kunizuia mimi,” alitamba Ame.
0 COMMENTS:
Post a Comment