Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm,
amemuondoa kiungo wake mshambuliaji, Mrisho Ngassa kwenye kikosi kitakachoivaa
Polisi Morogoro leo.
Yanga inatarajia kuvaana na Polisi Morogoro
katika mechi ya raundi tisa ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
Pluijm
alisema kuwa amemuondoa kiungo huyo kikosini kutokana na kutofanya mazoezi ya
pamoja na timu hiyo kwa siku mbili mfululizo katika kujiandaa.
Pluijm alisema sera yake ni kwamba mchezaji
asipofanya mazoezi ya pamoja na timu kwa siku mbili, ni vigumu kumtumia katika
mechi inayofuata, hivyo Ngassa hatakuwepo uwanjani kuwavaa Polisi Moro.
Aliongeza kuwa, kiungo huyo hakufanya mazoezi
ya pamoja na timu hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia aliyoyapata na
kusababisha kusafiri kwenda Tanga kuyamaliza.
“Mimi sera yangu ni kuwa mchezaji asiyefanya
mazoezi kwa siku mbili mfululizo, basi atakuwa amejiandoa kwenye kikosi changu,
kwa sababu hauwezi kumtumia mchezaji ambaye hayupo fiti.
“Ninaamini wapo wachezaji wengine
nitakaowatumia wenye uwezo mkubwa, Ngassa huenda akawepo kwenye mechi ijayo
baada ya kukamilisha matatizo hayo ya kifamilia,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment