MABOSI HAO WA ARSENAL WAKIWA NA MWENYEJI WAO NCHINI, IMAN KAJULA. |
Kama maofisa biashara wa Klabu
ya Arsenal wakifikia makubaliano mazuri na zaidi ya makampuni 20 ya hapa nchini, basi
timu shiriki za Ligi Kuu Bara, zikiwemo Simba na Yanga zitafaidika kwa udhamini
kutoka kwao.
Meneja Maendeleo na Uhusiano wa klabu hiyo, Daniel Willey, ameiambia SALEHJEMBE kuwa lengo kubwa ni kujenga mahusiano ya kibiashara kati ya Arsenal hapa
nchini.
Willey alisema wamepanga
kukutana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa ajili
ya kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya soka katika
kuhakikisha wanapiga hatua.
Aliongeza kuwa ni ngumu
moja kwa moja kukubali kuzisaidia klabu za ligi kuu kutokana na bodi maalum
Arsenal inayohusiana na maendeleo, hivyo hadi watakapokaa pamoja kujadiliana
ndiyo watatoa maamuzi.
“Tupo hapa nchini kwa ajili
ya kutengeneza masuala ya kibiashara kati yetu Arsenal na makampuni ya hapa
nchini, tulishaanza nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Nigeria, Kenya, Misri,
Afrika Kusini na nyingine nyingi ambazo tunauza vifaa mbalimbali vya michezo
zikiwemo jezi zetu kwa njia ya mtandao (online).
“Katika kujenga uhusiano
huo, tupo tayari kuzisaidia klabu za hapa nchini zinazoshiriki ligi kuu, lakini
hadi kutakapokuwepo makubaliano mazuri kati yetu na kampuni 20, tulizopanga
kufanya nazo biashara, tupo kwenye hatua nzuri za kukamilisha mpango,” alisema
Willey.
0 COMMENTS:
Post a Comment