Kocha wa Simba, Goran Kopunovic ameamua kuanza na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi.
Okwi ameingia kambini siku moja kabla ya Simba kushinda na kusonga hadi fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Taarifa za kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Okwi ataanza leo katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar.
"Ni kweli tumeambiwa Okwi ataanza, ila katika siku hizi mbili alizokuwa na sisi amefanya mazoezi kwa juhudi kubwa.
"Inaonekana hali hiyo imemvutia Kocha Kopunovic na msaidizi wake Matola, hivyo ataanza mechi yao leo," kilieleza chanzo ndani ya Simba.
Okwi ndiye alikuwa tegemeo la safu ya usambuliaji ya Simba katika mechi zote za Ligi Kuu Bara.
Hivi karibuni alirejea Uganda kwa ajili ya kufunga ndoa kabla ya kurudi kuichezea Simba katika mechi dhidi ya Kagera halafu akarejea tena mapumzikoni.







0 COMMENTS:
Post a Comment