January 13, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kikosi chake ni kikosi huru na hakuna mchezaji mwenye namba ya kudumu.


Pluijm raia wa Uholanzi amesema hana kikosi cha kudumu kwa kuwa kila baada ya mechi moja wanaanza upya kulingana na mechi inayofuata.

"Huwezi kuwa na mchezaji mwenye namba fulani. lazima wachezaji wajitume na wajue akishuka mwenzake anachukua nafasi.

"Napenda kuwa na kikosi huru ambacho kila mmoja atapata nafasi ya kukichezea kutokana na juhudi zake na namna anavyofanya vizuri," alisema.

Tayari Yanga imeingia kambini mjini Bagamoyo kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara.

Lakini tayari Yanga imeanza maandalizi ya mechi yake ya kimataifa ya Kombe la Caf dhidi ya BDF ya Botswana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic