Kitendo cha beki wa Ruvu Shooting, George
Michael kumpiga kabala ya koo mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe hivi
karibuni wakati timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kimeendelea
kuwa gumzo na sasa kimevuka mipaka ya Tanzania.
Nchini Burundi anakotokea Tambwe, jambo hilo
limekuwa gumzo kubwa lakini pia baadhi ya wachezaji wanaocheza ligi kuu ya nchi
hiyo, wamekuwa wakitumiana kwa njia ya mtandao picha ambazo zilipigwa na gazeti
hili zikimwonyesha Tambwe akipigwa kabali na Michael.
Mchezaji wa
zamani wa Inter Stars ya Burundi, Ndayishimiye Duni, alisema kuwa kitendo hicho
kiliwashangaza watu wengi nchini humo, hususan wachezaji.
Alisema kila mtu anaona kuwa, Tambwe
hakutendewa haki na beki huyo kwa kumpiga kabala, jambo ambalo ni kinyume na
taratibu za soka, hivyo wanalitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kumchukulia hatua.
“Lakini pia maneno ambayo alikuwa akitukanwa
na beki huyo, kwa kumuita mkimbizi pia siyo mazuri, yanalichafua soka la
Tanzania na kuonekana halina Fair Play.
“Hata hivyo wachezaji wengi nchini hapa
wamewasiliana na Tambwe na kumpatia pole kutokana na tukio hilo baada ya kuona
picha ambazo tulizipata kutoka katika mtandao wa Gazeti la Championi (Global
Publishers),” alisema Duni.
Alipoulizwa Tambwe juu ha suala hilo, alisema:
“Ni kweli kabisa wachezaji wengi kutoka Burundi wamekuwa wakinipigia simu na
kunipatia pole kutokana na jambo hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment