Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi
karibuni ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa January Makamba, ameweka wazi shauku yake ya kuinua kiwango cha
michezo nchini.
Makamba ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wenye
mvuto mkubwa kwa vijana nchini, aliweka wazi nia yake hiyo katika mazungumzo
yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho
gazeti hili limepata nakala yake.
Mbunge
huyo amesema anataka kujenga vituo vya michezo vya kanda vyenye hadhi ya olimpiki.
“Inafedhehesha
sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya
mwisho tumeshiriki katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
“Mwaka huohuo wa 1980, ndiyo ilikuwa mara ya
kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu mzee
Suleiman Nyambui na mzee wetu Filbert Bayi ndiyo walitutoa kimasomaso kipindi
kile. Ni muhimu kurekebisha hili,” alisema Makamba katika kitabu hicho.
Kama mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya
kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu, Makamba anaungwa
mkono na vijana wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na
kuepuka malumbano ya jukwaani.
Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa urais
kuweka bayana mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi.
“Tufikie
wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia sasa na
serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo ili kuziwezesha kukaa kambini,
kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha kushiriki kikamilifu katika
mashindano ya kimataifa,” alimalizia Makamba alipokuwa akigusia mpango wake wa
kuinua michezo nchini.
Shida ni as if michezo ni mpira wa miguu tu naamini bado tuna tatizo kubwa hapo kama Jk uwekezaji wake ungekua kwenye riadha naamini tungukiwa tunazungumza lugha tofauti kabosa
ReplyDelete