Msanii nyota wa Hip Hop nchini, John Simon ‘Joh Makini’, amefunguka
kuwa licha ya kujikita katika muziki lakini pia ni mpenzi mkubwa wa soka ambapo
yeye ni shabiki ‘damu’ wa Simba.
Joh Makini anayetamba na nyimbo za Najiona Mimi na Gere, amefunguka
kuwa amekuwa akifuatilia soka japo siyo kwa ukaribu lakini Simba ndiyo timu
ambayo ipo kwenye damu yake.
“Mimi ni shabiki wa Simba kwa hapa nyumbani na nimekuwa
nikiifuatilia timu yangu, nje ya nchi sina timu ya kushabikia zaidi nashabikia
mchezaji mmoja-mmoja, tena hasa Waafrika tu.
“Na kuhusu Simba kutimua kocha siwezi jua sababu yao hasa, viongozi
ndiyo wanaotambua nini kilichokuwa nyuma ya pazia lakini kwa upande wa Yanga
najua kipigo cha Nani Mtani Jembe ndicho kilichosababisha kufukuzwa Marcio
Maximo,” alisema Joh Makini.
0 COMMENTS:
Post a Comment