Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, amelalama kuwa maumivu ya
nyonga yanamtesa kiasi cha kushindwa kurejea dimbani na kudai kuwa maumivu hayo
yamekuwa yakimwandama mara kwa mara.
Tegete ambaye ameshindwa kucheza mechi hata moja katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi, ameliambia gazeti hili kuwa, amekosa amani na furaha
kutokana na majeraha hayo ambapo hata akipona anajikuta anajitonesha hivyo kuanza
kujiuguza tena.
Amedai kuwa anaendelea kupata matibabu huku akifanya programu ya
mazoezi binafsi ya kukimbia ufukweni kila asubuhi na jioni.
“Ninakosa amani kabisa juu ya majeraha haya ya nyonga, inafikia
kipindi ninafikiria au ninasumbuliwa na jeraha lingine tofauti na nyonga?
Lakini ndiyo hivyo mipango ya Mungu,” alisema Tegete huku akionekana kuwa
mnyonge.
0 COMMENTS:
Post a Comment