Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
amekumbana na balaa mjini Musoma.
Julio amepigwa jiwe na kujeruhiwa wakati
timu yake ya Mwadui FC ikicheza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Polisi
Mara.
Mechi hiyo ilichezwa wikiendi mjini Musoma
na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Hali hiyo ilisababisha mashabiki wa Polisi
kuanza kuwashambulia Julio na wachezaji wake ambao baadhi walijerudiwa.
“Kweli nimepigwa jiwe la mgongoni na sasa
siko vizuri. Nimeshindwa hata kwenda mazoezini.
“Hakika hawakututendea haki na askari polisi
hawakuwa na msaada,” alisema Julio.







0 COMMENTS:
Post a Comment