Dakika chache baada ya kutwaa tuzo ya mchaji bora wa dunia, maarufu kama Ballon d'Or, Cristiano Ronaldo amefunga wazi kwamba anataka kumfikia Lionel Messi.
Ronaldo ameeleza kufurahishwa kwake na kutwaa tuzo yake ya tatu lakini akasisitiza angefurahi kuichukua kwa mara ya nne kama ilivyo kwa Messi.
Ronaldo ameshinda tuzo hiyo mara mbili mfululizo lakini kabla aliibeba mwaka 2008 akiwa Manchester United.
Messi wa Barcelona ameishachukua mara nne lakini kwa mwaka wa pili mfululizo ameshindwa kufua dafu mbele ya Ronaldo wa Real Madrid.









0 COMMENTS:
Post a Comment