Hatua
ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa kesho
(Januari 26 mwaka huu) na Januari 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex
uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kila siku.
Mechi
ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam
Televisheni itaanza saa 9 alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo
fainali ya pili ambayo ni kati ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.
Ilala
na Iringa watacheza robo fainali ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9
kamili alasiri, na kufuatiwa na robo fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni
itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.
Nusu
fainali za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari
29 mwaka huu wakati Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15
jioni ambapo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).
Timu
zote zilizoingia hatua hiyo ya nane bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara
ya kwanza nchini zimefikia hosteli ya Msimbazi.
Wakati
huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na
waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5
asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
0 COMMENTS:
Post a Comment