January 25, 2015

PLUIJM AKIWA NA BENCHI LAKE LA UFUNDI...
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema licha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro, bado hawajapata wanachotaka.


Pluijm raia wa Uholanzi ameiambia SALEHJEMBE, kwa kiasi fulani kikosi chake kilicheza vizuri katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro lakini si kama walivyotaka.

"Utaona, bado tumeendelea kupoteza nafasi za kufunga. Jambo ambalo limekuwa likitusumbua sana.

"Ndiyo maana nasema bado hatujapata tunachotaka na katika soka, kila siku ni mpya na unajifunza tena," alisema.

Yanga iliishinda Polisi Moro, lakini wachezaji wake walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic