January 25, 2015



MPIRA UMEKWISHAAAA....

Dk 90+3 Simba wanapata kona nyingine
Dk 90+2 Simba wanapata kona
Dakika 4 za nyongeza

Dk 90, Kisiga anapiga faulo lakini mpira unatoka juu ya lango.
Dk 84 Azam wanafanya shambulizi kali lakini Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa.

Dk 82, Mcha anapiga shuti kali lakini Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa kabla ya mabeki kuondosha mpira.
Dk 79, Morris anapoga shuti kali sana lakini linatoka nje kidogo ya lango.

Dk 78, Himid na Kessy wote wanalambwa kadi za njano kwa kuchezeana madhambi.Dk 72, mechi inaonekana kuchafuka na wachezaji wanachezeana kibabe, mwamuzi anamlaba kadi ya njano Mcha Ali

Dk 69, Simba wanamtoa Ndemla anaingia mkongwe shabaki Kisiga.

Dk 65, Awadhi Juma anaingia kuchukua nafasi ya Okwi ambaye ameumia.

Dk 64, Bocco anapiga shuti kali linakwenda mikononi mwa kipa Manyika.
Dk 60, Okwi aanaumia, anatibiwa lakini inasindikana na inaelezwa amepoteza fahamu anaingizwa vyumbani akiwa amebabwa na madaktari.


GOOOOOOOO Dk 57, Azam FC anafunga bao la kusawazisha baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe. Anapiga shuti kali 

Dk 54, Azam wanamtoa Kavumbagu wanamuingiza John Bocco.
toa 

Dk 47, Simba ndiyo wanaonekana kuanza mashambulizi kwa kasi katika kipindi cha pili.
Dk 45, Simba wanamtoa Maguli anaingia Simon Sserunkuma na Azam wanamtoa Domayo anaingia Mcha Hamisi.

MPIRA MAPUMZIKO:


Dk 42 Kapombe anapiga shuti lakini inazuiwa na kuwa kona inayochongwa na Kipre anapiga juuuuu
Dk 36, Messi Singano anawatoka mabeki wa Azam na kutoa pais nzuri lakini wenzake wanashindwa kuwa makini.


Dk 32, Kipre anatoa bonge la pasi kwa Kavumbagu, lakini anapiga shuti kuuubwa juu


Dk 29, Azam FC inafanya shambulizi kali Tchetche anapiga shuti linaokolewa na mabeki wa Simba wakati likiwa limempita kipa Manyika.

Dk 25, Simba wanafanya shambulizi kali, lakini Ndemla anashindwa kumalizia akiwa analitazama lango la Azam
Dk 22, Kavumbagu anamjaribu Manyika, lakini anashindwa kulenga lango.


GOOOOOOOOO Dk 19, Okwi anafunga bao baada ya 'kumchungulia' kipa Mwadini Ally
Dk 15 Kipre anawatoka mabeki wa Simba na kupiga krosi kwa Kavumbagu anayeunganisha lakini Manyika anafanya kazi ya ziada kudaka.


Dk 10, Singano anapiga krosi safi lakini Azam FC wanaokoa
Dakika ya 5, Ramadhani KESSY anapiga shuti kali lakini Mwadini Ally anadaka.



Dakika ya 1, Kipre Tchetche anaingia na mpira na kupiga krosi 'isiyokuwa na macho'.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic