Uwezo mkubwa wa kukaba na kucheza mipira ya
vichwa alionao beki wa kati wa Simba, Mganda, Juuko Murushid, umemfanya kocha
mkuu wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic amfanananishe na beki kisiki wa
Barcelona na timu ya taifa ya Serbia, Nemanja Vidic.
Murushid amekuwa gumzo tangu ajiunge na Simba msimu
huu kutokana na uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya mafowadi, hali ambayo imemfanya
kocha wake aamue kumpa jina jipya la Vidic kutokana na kazi anayopiga.
Kopunovic
amesema kuwa, Murushid ni mmoja wa mabeki anaowaamini katika kikosi chake kwa
sasa.
Aliongeza kuwa, uwezo wake mkubwa wa kukaba na
kupiga mipira ya vichwa ni kama alivyokuwa Vidic ambaye sasa anakipiga katika Klabu
ya Inter Milan ya Italia.
“Juuko ni beki mzuri mwenye uwezo mkubwa wa
kukaba na kupiga mpira ya vichwa vizuri sana utafikiri ni Vidic, hivyo
najivunia kuwa naye katika kikosi changu.
“Ni matumaini yangu uwepo wake kwa sasa
utatusaidia kufanya vizuri zaidi katika mechi zetu za ligi kuu, ikiwemo ile
tutakayocheza hivi karibuni dhidi ya Azam,” alisema Kopunovic.
0 COMMENTS:
Post a Comment