January 10, 2015


 
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amewataka wachezaji wake kufunga mabao ya mapema.

Katika mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Polisi Zanzibar katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, leo, Kopunovic amesisitiza mabao ya mapema na hasa kipindi cha kwanza.

Kocha huyo raia wa Serbia amesisitiza kwamba lazima timu hiyo izitumia nafasi mapema ili kulahisisha kipindi cha pili.

Simba inawavaa Polisi, leo usiku katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu baada ya maafande hao kuwavua ubingwa KCCA ya Uganda na kuwang'oa katikaa hatua ya robo fainali.

Katika mazoezi ya Simba, mara nyingi kocha huyo alikuwa akiwanoa wachezaji wake namna ya kuipita na kuihadaa ngome ya timu pinzani.

Lakini umakini pia upande wa makipa kwa ajili ya kuusoma mchezo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic