Kiungo Mesut Ozil atarejea
uwanjani kesho wakati Arsenal inakipiga dhidi ya Stoke City.
Ozil inarejea Ligi Kuu
England baada ya kukaa nje miezi mitatu kutokana na maumivu ya goti.
Kocha Arsene Wenger amesema
Ozil amekuwa akifanya mazoezi na wenzake na sasa yuko fiti, hata hivyo
inaonekana ataanzia benchi.
Mjerumani huyo aliyejiunga
na Arsenal akitokea Madrid aliumia katika mechi dhidi ya Chelsea, Oktoba mwaka
jana.
Ozil ndiye mchezaji ghali
zaidi Arsenal iliyompata kwa kitita cha pauni milioni 42.5.
0 COMMENTS:
Post a Comment