Siku chache baada ya beki wa kati wa Simba,
Joseph Owino, kutua nchini ili kuendelea na kazi yake ya kuitumikia klabu hiyo,
amekumbwa na balaa ambalo linaweza kumkosesha amani katika kipindi chake chote
kilichobakia klabuni hapo.
Balaa hilo linatokana na kocha mkuu wa timu
hiyo, raia wa Serbia, Goran Kopunovic kudai kuwa hana mpango na mchezaji huyo
katika kikosi chake kwa hivi sasa kwa sababu hamjui na hajawahi kumuona hata
siku moja akiwa uwanjani.
Kopunovic
amesema kuwa kwa sasa akili yake yote ameielekeza kwa wachezaji waliopo katika
kikosi hicho ili kuhakikisha wanakuwa fiti na kutimiza malengo yake ya muda
mfupi aliyojiwekea.
“Siwezi kukaa namfikiria mchezaji mmoja ambaye
hata simjui na sijawahi kumwona uwanjani akicheza kama ilivyo kwa wengine
katika kikosi changu.
“Kama angekuwa anapenda kazi basi asingechelewa
kuja kuendelea na kazi yake baada ya kumalizika kwa muda wake wa mapumziko,”
alisema Kopunovic.
0 COMMENTS:
Post a Comment