Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kutangaza kumfungia mshambuliaji wa Stand United, Haruna Chanongo kucheza mechi
tatu na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 kwa madai ya kumpiga teke
mwamuzi katika mchezo dhidi ya Polisi Moro, uongozi wa Stand umekata rufaa
kupinga.
Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la Stand, Muhibu
Kanu amesema wamesikitishwa na maamuzi hayo, ndiyo maana wameamua kukata rufaa
kwa kuwa Chanongo hakumpiga mwamuzi huyo teke.
Alisema wameshatuma video ya mchezo huo na
barua kwenda kwa kamati ya nidhamu ya TFF ili kupitia video kwa umakini.
“Chanongo ni mchezaji mzoefu, hawezi kufanya
kitu kama hicho, tunaamini haki itatendeka,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment