Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amekubali
kuwa kikosi cha Azam FC ni kati ya vilivyo bora nchini katika soka.
Lakini akahoji, nani ambaye anasema Simba ina
kikosi dhaifu na haiwezi kuifunga Azam leo?
Simba na Azam FC zinakutana leo katika mechi ya
“big match” za Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kocha huyo raia wa Serbia amesema, kikosi chake
kina uwezo mkubwa wa kupambana.
“Tunataka kupambana na kushinda, tunataka pointi
tatu kwa ajili ya kujiweka vizuri kwenye msimamo.
“Lakini vizuri tushinde ili kuondoa hizo hisia
kikosi chetu ni dhaifu, njoo uone tunacheza,” alisema
0 COMMENTS:
Post a Comment