January 24, 2015


Mabosi wa mabenchi ya ufundi katika vikosi vya Simba na Azam wametambiana kuwa hawahofii mechi ya kesho wakati timu hizo zitakapomenyana katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.



Kocha wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, ametamba kuwa Azam anawafahamu vilivyo hivyo hawatamsumbua katika mchezo huo, kauli ambayo pia imetolewa na Joseph Omog wa Azam kwa kusema kuwa amekutana na Simba mara kadhaa, hivyo hawampi shida.

Kopunovic amesema kuwa, amewashuhudia Azam wakicheza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, hivyo atahakikisha katika mchezo huo anaibuka na ushindi.

“Azam niliwaona wakicheza kwenye Mapinduzi, tayari nimewaandaa vijana wangu kuweza kukabiliana nao na ninaamini hawatatusumbua,” alisema Kopunovic huku Omog akijibu mapigo kwa kusema:

“Tumekutana mara kadhaa na Simba, siwezi kuwa na hofu yoyote na mchezo huo, cha msingi vijana wangu wamejiandaa vema, kinachosubiriwa ni mechi tu uwanjani.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic