ULINZI! Uwanja wa Jamhuri
ambao utatumiwa kwenye mechi kati ya wenyeji Polisi Morogoro na Yanga leo,
umeripotiwa kuwekwa chini ya ulinzi na askari wakihofia kuwekwa ndumba.
Askari hao walianza kazi
hiyo kwa siku tatu nyuma wakiihofia Yanga kuweza kufanya mambo hayo ya
Kiswahili.
Katika mazoezi ya jana
kwenye uwanja huo, Salehjembe liliwashuhudia askari wakiwaondoa
mashabiki na wanachama wa Yanga ili waendelee kuweka ulinzi.
Hata hivyo, askari hao
walimdaka kijana mmoja shabiki wa Yanga aliyeonekana akiweka vitu kwenye ‘pichi’
na walipomkagua walimkuta na ndimu pamoja na chumvi kwenye mfuko wa nguo yake
kabla ya kumsweka selo.
Katibu Mkuu wa Tawi la
Yanga Morogoro Mjini, Edward Mhagama, alithibitisha hilo na kudai kijana huyo
alikuwa na vitu hivyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
0 COMMENTS:
Post a Comment