Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda
ameifungia timu yake bao pekee dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, Mrwanda
alifunga bao hilo dakika ya 42 dhidi ya timu yake ya zamani akiunganisha krosi
safi kutoka kulia mwa uwanja.
Kipindi cha kwanza kilionekana kuwa ni ‘mali’ ya Yanga ambayo ilishambulia zaidi lakini wachezaji wake walipoteza nafasi nzuri kufunga.
Kipindi cha pili, Polisi wakaonekana
kuimarika na kushambulia zaidi ingawa nao hawakuwa makini katikam ufungaji.
Mliberia, Kpah Sherman naye alionekana kuwa
mwiba kwa mabeki wa Polisi.
Hata hivyo beki mkongwe, Lulanga Mapunda
aliongoza vizuri safu yake ulinzi ya Polisi kuhakikisha hairuhusu bao tena.
0 COMMENTS:
Post a Comment