Msanii nyota wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
amefunguka kuwa katika soka la kimataifa, mchezaji wake kipenzi ni Samuel Eto’o
anayekipiga Everton ya England.
Diamond ambaye alitarajiwa kutumbuiza katika utoaji Tuzo za
Mwanasoka Bora wa Afrika 2014, zilizofanyika jana nchini Nigeria, amesema
anaheshimu uchezaji wa Eto’o ambaye kwa sasa amestaafu kuitumikia timu yake ya
taifa ya Cameroon.
“Namkubali sana Eto’o, jamaa anajua anachokifanya na ameiwakilisha
vizuri Tanzania,” alisema Diamond kwa njia ya simu.
Akizungumzia kuwakilisha Tanzania katika sherehe hizo, Diamond
alisema: “Nimefurahi kupita kiasi, hii inaonyesha ni kwa jinsi gani muziki wetu
umekua hadi Afrika Kusini kutaka kuwa na moja ya vionjo katika tamasha kubwa
kama hilo, sikuwahi kufikiria ipo siku nitaiwakilisha nchi yangu kwenye tuzo
kubwa kama hizi.”









0 COMMENTS:
Post a Comment