January 8, 2015


Yanga imeng'oka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na JKU.

Muuaji wa Yanga alikuwa Amour Mohammed ambaye alifunga bao katika dakika ya 72 na kuwapa Yanga wakati mzuri wa kusawazisha bila ya mafanikio.

JKU inayomilikiwa na Jeshi la Zanzibar imefanikiwa kuing'oa Yanga kwa bao hilo moja katika mechi kali na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kutokana na ushindi huo, sasa JKU itacheza nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo iliing'oa Azam FC leo mchana.

Yanga ilipoteza nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha kwanza.

Lakini JKU walionekana kuwa tofauti na kucheza soka la kuvutia tokea mwanzo wa kipindi cha kwanza huku wakichezaji wake wakionana kwa pasi za uhakika zilizoonyesha kuna kitu wanatafuta.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic