Na Saleh Ally
NIMECHAMBUA mambo kadhaa kuhusiana na mechi ya
Nani Mtani Jembe iliyowakutanisha watani, Simba wakashinda kwa mabao 2-0 dhidi
ya Yanga.
Mechi hiyo ya mwishoni mwa mwaka jana ilifana
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Siku chache baadaye nikaanza kuhoji kuhusiana na
mapato kwa kuwa hayakutangazwa, kwa nini ilikuwa siri?
Nilitaka kujua kuhusiana na mgawo na Yanga na
Simba zilifaidikaje kwa kuwa inaonekana wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro,
walichukua kiasi cha fedha. Swali likawa vipi wadhamini wahusike na kuchukua
mapato? Sikupata jibu.
Safari hii, si mimi. Ni mashabiki wa soka
waliopata nafasi ya kutoa maoni yao kupitia ujumbe mfupi. Wapo ambao
wamethubutu kuita ukimya wa kutotaja mapato hayo ni sawa na ile kashfa
iliyotawala vyombo vya habari nchini, Escrow.
Wapo waliosisitiza Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), wengine Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wafanye juhudi kuhakikisha
mapato yanatangazwa.
Nimepokea zaidi ya meseji elfu moja, lakini
kwa kuchukua mmoja kwenda mwingine, hawa wachache wamepata nafasi ya kutoa
maoni yao na nitaendelea kuwapa nafasi wengine pia kadiri nafasi
itakavyopatikana:
Viongozi wa Afrika siyo kwenye michezo tu bali
kila kona wanaweza kuchakachua, hapa kuna kulindana sana wala hawawezi kutoa
majibu ya mapato ya Nani Mtani Jembe, kila mtu ameshajikatia chake.
Man Jack wa Dar- 0652 204442
Kiukweli jamaa wanazingua mpaka leo hatujui
pesa za mapato ziko wapi, usichoke kaka, pambana mpaka tuupate ukweli.
Twahiri Omary wa Tandika-0784 680266
Kwanza nakupongeza kwa kuwa mkweli kwa kufuatilia
suala hili, umekuwa mtu wa kwanza kuuliza juu ya mapato ya mechi hiyo tofauti
na vyombo vingine vya habari, unachouliza ni haki yetu wapenzi wa soka.
Amiri Juma wa Tandika-0717 208711
Hata wakitoa bastola wang’ang’anie mpaka waseme
ukweli, fedha kachukua nani? Hao ni Escrow wa soka.
Abubakar Hamidu wa Chamazi-0717449887
Tunataka kufahamu nani wanatuibia fedha zetu,
klabu nazo watueleze, kama hawajapewa mapato ya mlangoni itakuwa haina maana ya
kucheza mechi kama hizo.
Khamisi Omary wa Kitunda- 0773 064753
Napata hofu katika suala hili la mapato ya
Nani Mtani Jembe, yaani ukiangalia kwa undani nahisi kuna ujanja umefanyika
kati ya TBL, klabu na TFF, pambana kaka mpaka kieleweke.
Salum Makamba wa Kigogo-0716 884284
Ni kweli timu zetu zinanyonywa sana katika
mapato ya mechi ya Nani Mtani Jembe.
John Kajembe wa Muheza- 0714 634545
Nionavyo, mgawo wa mechi hiyo umeliwa na
baadhi ya viongozi wa juu wa soka, ndiyo maana hatupati majibu sahihi ya mapato
hayo.
Hemed wa Turiani- 0755 513054
Kiukweli TFF ndiyo wanatakiwa kutupa majibu
sahihi juu ya mapato yote yaliyopatikana kwenye mchezo huo.
Emmanuel Nyika wa Mbeya- 0754 431852
Sisi tutakuwa nyuma yako daima katika
kukusapoti mpaka tujue hizo fedha zimesaidia nini katika sekta ya michezo hapa
nchini.
Cheche Idd wa Morogoro-0657 380198
Nakuunga mkono katika hilo, tunaomba
tujulishwe hiyo Escrow ya soka ni akina nani wanaisimamia.
Alberth Tezura- 0767-636317
Inabidi ifike kipindi klabu hizo mbili zichoke
kuburuzwa, haiwezekani ziingie zaidi ya milioni 600 halafu timu zipewe milioni
7, hapo lazima tuhoji fedha zinaenda wapi.
Nimrodi wa Makambako-0759 564936
Naona fedha za Mtani Jembe kama zilishaliwa
hata kabla ya mechi yenyewe.
Baba Rahman wa Mbezi Beach-0717 220051
Katika suala hili la TBL, naomba usichoke,
lifuatilie na sisi hatutachoka kusoma makala zako.
Amiry wa Zanzibar-0715 083206
Yaani ikiwezekana twende wote huko TBL
tukaulizie wote kuhusiana na sakata hilo, huu siyo muda wa kumuogopa mtu
yeyote.
Abdu Kirobo wa Mbagala, Dar- 0713-923168
Komaa kaka mpaka tujue fedha hizo zimeenda
wapi na kufanya nini na kwa faida ya nani?
Said wa Kigoma-0714 815641
Mimi napendekeza ikiwezekana hata tufanye
maandamano tujue hizo fedha zimeenda wapi.
Jay Meli wa Dar-0785 304209
Naomba kuungana na wewe, hivi hata wanachama
na mashabiki wa Yanga na Simba hawana macho na masikio katika hili suala la
Nani Mtani Jembe?
Matemba wa Mwanza-0787 169802







0 COMMENTS:
Post a Comment