Mshambuliaji wa Simba Dan
Serrunkuma amegeukwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kupokelea kama mfalme
kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Sserunkuma alisajili na
Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya baada ya kuibuka mfungajili bora wa Ligi Kuu
ya nchi hiyo, lakini ameshindwa kuendeleza cheche zake kwa Wekundu hao wa
Msimbazi.
Juzi Jumapili mchezaji huyo
alionja joto ya jiwe baada ya kuzomewa na mashabiki kutokana na kuonyesha
kiwango kibovu kwenye mchezo dhidi ya JKU ya visiwani hapa ambao Simba walipata
ushindi wa bao 1-0.
Hata hivyo kitendo hicho
kuzomewa mchezaji huyo kilimsikitisha mchezaji huyo ambaye alisema kwamba:
“Ila soka ndiyo hivyo lilivyo lakini naomba niwaambie
mashabiki wa Simba kuwa wawe na subira mambo yatakuwa vizuri tu japokuwa kwa
sasa sijisikii vizuri,” alisema Sserumkuma.







0 COMMENTS:
Post a Comment