MBEYA CITY |
Katika kuhakikisha unaivuruga Tanzania
Prisons, uongozi wa Mbeya City umesema utahakikisha unacheza soka la kasi muda
wote ili kuhakikisha wanapata mabao ya mapema.
Timu hizo zinatarajia kukutana kesho Jumapili
katika mchezo unaotajwa kuwa ni derby ya Mbeya ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine,
Mbeya.
Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema
sasa kikosi hicho kina morali kubwa tofauti na mwanzo ambapo walikuwa wanawachukulia
poa.
“Sisi tumejiandaa vizuri ili kuhakikisha
tunachukua pointi zote tatu bila kujali kama timu zote ni za nyumbani au la! Awali
hatukuweza kubaini matatizo ambayo yanaikumba klabu, lakini sasa kazi ya kocha
imeanza kuzaa matunda hali ambayo inaleta matumaini ya kurejea kwenye chati nzuri.”
Naye Kocha wa Prisons, David Mwamwaja,
alisema: “Tumejindaa kuhakikisha tunashinda licha ya kuwa mvua zinanyesha sana
ukanda huu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment