Mbeya City na Prisons zimemaliza mchezo wao wa upinzani mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara kwa mabao 2-2.
Sare hiyo imemaliza ubishi katika mchezo huo wa watani wa jiji la Mbeya.
Prisons ilifanya kazi ya kusawazisha kila bao baada ya Paul Nonga kuanza kuifungia Mbeya City, wakasawazisha na Themi Felix akafunga la pili nao wakajibu.
Mbeya City walionekana kung'ara zaidi katika kipindi cha pili lakini mambo hayakuweza kuwa mazuri zaidi ya sare.
0 COMMENTS:
Post a Comment