Wakati kikosi cha Mbeya
City kikiendelea kujifua kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu Bara, sasa wameelezwa
kuwa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ni wa raundi ya 11 utachezwa katika
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, badala ya Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Mbeya City katika raundi ya
tisa na kumi haitakuwa na michezo ya ligi kuu ambapo walitakiwa kuwavaa Simba
na Yanga baada ya michezo hiyo kusogezwa mbele kutokana na timu hizo kuwa
Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo unaotarajiwa
kupigwa Januari 17, mwaka huu umehamishiwa Mwanza kutokana na marekebisho
yanayofanywa kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Ofisa wa Mbeya City, Dismas Ten, alisema kwa sasa kikosi chao
kinaendelea kujifua kwa siku mara mbili ili kuwa imara zaidi baada ya kupata muda zaidi wa
kujiandaa.
“Kwa sasa tunaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wetu dhidi
ya Kagera, ambapo uwanja wao wa nyumbani umehamishiwa Mwanza kutokana na ule wa
Kaitaba kufanyiwa ukarabati, lakini hatuna tatizo katika hilo na tutakwenda
huko huko.
“Zaidi kwa sasa mwalimu (Juma
Mwambusi) anaendelea kukinoa kikosi chake kwa ufasaha ili kuweza kukijenga kiwe
bora na kufanya vizuri,” alisema Ten.







0 COMMENTS:
Post a Comment