Kocha wa makipa wa Yanga,
Juma Pondamali amepigwa marufuku kujihusisha na shoo za muziki mpaka pale ligi
kuu itakapomalizika msimu huu.
Kocha huyo asiyeishiwa
vituko, amekuwa akijihusisha na masuala ya muziki na mpaka sasa ameshatoa ‘singo’
kadhaa ikiwemo Domo la Mamba na nyingine kibao.
Kocha huyo alisema amepigwa marufuku na uongozi wa timu hata kama
kuna sikukuu, biashara za kwenda kufanya shoo na kupanda jukwaani zisifanyike
kwa sasa.
Pondamali alifunguka zaidi
na kudai hana jinsi inabidi asikilize viongozi wake wanataka kitu gani, hivyo
mashabiki wake wamsubiri kwanza.
“Kwa sasa viongozi wangu
hawataki kabisa kusikia wala kuniona jukwaani nafanya shoo hata kama kuna
sikukuu au nimepata mualiko, zaidi wamesema nisubiri tu mwezi Mei ambapo ligi
itakuwa imesimama.
“Kwa hiyo kwa sasa hakuna
kinachoendelea, hivyo nasubiri hiyo Mei ligi itakapomalizika ndiyo nitarudi mzigoni
kuendelea na majukumu yangu ya kutoa album na video za nyimbo zangu,” alisema
Pondamali.







0 COMMENTS:
Post a Comment