January 8, 2015

POLISI WAKISHANGILIA BAADA YA KUING'OA KCCA KWENYE ROBO FAINALI
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Polisi Zanzibar, haitakuwa lelemama.

Polisi inakutana na Simba katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Amaan, mjini hapa Jumamosi.
KOPUNOVIC NA MSAIDIZI WAKE SELEMANI MATOLA.
Kopunovic amesema Polisi imekuwa ikiendelea kuimarika na kusema walionyesha mchezo mzuri wakati wakiing'oa na kuivua ubingwa KCCA ya Uganda.

"Lakini kikosi chetu pia kinabadilika kwa kuwa kadiri siku zinavyokwenda kuna mambo tunaendelea kujifunza.

"Hata sisi tutakuwa na mabadiliko makubwa na tunachotaka ni kushinda ili tupate mechi nyingine ya kujiandaa zaidi na ligi.

"Kikubwa kinachovutia ni ushindani mkubwa wa michuano ya Mapinduzi na sisi tunaendelea kujiandaa," alisema Kopunovic.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic