January 10, 2015


Nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, amefunguka kuwa anaipa nafasi kubwa timu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kutokana na timu zilizobaki.


Yanga imeondolewa katika Kombe la Mapinduzi hatua ya robo fainali huku wapinzani wao, Simba wakitinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Jang’ombe.

Myarwanda huyo anaamini baada ya Simba, anaipa nafasi ya pili Mtibwa Sugar.

“Kwa jinsi timu zilivyobaki naipa nafasi kubwa Simba kutwaa ubingwa ikifuatiwa na Mtibwa kwani ndizo timu ninazoziona kuwa na ushindani zaidi,” alisema Niyonzima.


 Niyonzima ni kati ya wale waliofanya vizuri kwenye Kombe la Mapinduzi.

Yanga imeng'olewa ikiongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi ikiwa na mabao 9 na pointi 9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic