Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amefunguka kuwa tangu
aanze kufundisha soka miaka 19 iliyopita, hajawahi kushuhudia kitendo cha kishirikina katika soka
kama ilivyotokea hivi karibuni katika mchezo wao dhidi ya Shaba.
Jumanne iliyopita, mwanachama wa Yanga maarufu kwa jina la Carlos,
aliingia uwanjani pembeni ya lango la wapinzani na kuchukua glovu za akiba za
kipa wa Shaba, Bakari Shaweji kisha kukimbia nazo ikiwa ni katika dakika ya 81,
ambapo dakika tano baadaye Andrey Coutinho aliifungia Yanga bao zuri.
Kocha huyo alifunguka kuwa tangu aanze kufundisha mwaka 1996
barani Afrika tukio hilo lilimshangaza zaidi.
“Mambo ya kishirikina yanachangia soka la Afrika kurudi nyuma kwa
kiasi kikubwa na kupoteza saikolojia ya wachezaji uwanjani, hasa tukio
linapotokea mpira ukiwa unaendelea uwanjani si vyema sana,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment