January 6, 2015


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema pamoja na timu yake kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Mapinduzi angepelea kuona inashinda mechi ya leo.


Yanga inashuka kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar leo saa 2 usiku kuivaa Shaba.

Pluijm raia wa Uholanzi amesema wakishinda mabao manne tena litakuwa jambo jema, lakini zaidi itakuwa poa zaidi.

"Mabao manne tena! sawa, litakuwa jambo zuri zaidi. Ikiwezekana tano, sita au zaidi. Michuano hii ni sehemu ya kujiimarisha kwa ajili ya ligi ya nyumbani na michuano ya kimataifa," alisema.

Yanga imeanza michuano hiyo kwa kushinda mabao nane katika mechi zake mbili za mwanzo za kundi.

Ilianza kwa kuitandika Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0, halafu ikarudia ushindi wa idadi hiyo dhidi ya Polisi Zanzibar.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic