January 13, 2015


MTIBWA:
Ally Lundenga (pata)
Shabaki Nditi (pata)
Rajab Jeba (kosa)
Ramadhani Kichuya (pata)
Vicent Barnabas (kosa)

SIMBA:
Awadhi Juma (pata)
Shabani Kisiga (kosa)
Ramadhani Kessy (pata)
Hassan Isihaka (pata)
Danny Sserunkuma (pata)






DAKIKA 90 ZIMEKWISHA:
Dk 90+2 Manyika anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Ivo Mapunda

Dk 90+1 Mtibwa inamtoa Ame Ally na anaingia Abdallah Juma
Dk 88, mpira wa adhabu wa Kessy unaokolewa na kipa Said
Dk 86 Ndemla anagongwa na Jeba, analazimika kutolewa nje ya uwanja baada ya kutibiwa. Nafasi yake inachukuliwa na Shabani Kisiga.

Dk 81 Messi anawachambua mabeki wa Mtibwa, anapiga shuti inakuwa kona isiyo na matunda

Dk 78 Mgosi anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Vicent Barnabas..

Dk 77 Mussa Mgosi anapewa kadi ya njano baada ya kumkwatua Kessy
Dk 75, Simba wanamtoa Okwi naa nafasi yake inachukuliwa na Awadh Juma

Dk 68, Mtibwa inapata kona tatu mfululizo lakini hata hivyo hazizai bao
Dk 66 Anaingia Jeba kuchukua nafasi ya Chiwawa upande wa Mtibwa.

Dk 65 anatoka Ajib anaingia Elius Maguli
Dk 64, Ajibu anapiga tik tak lakini Said anadaka


Timu zote zinaanza kwa kushambuliana kwa zamu na mpira unaonekana kuchezwa zaidi katikati zaidi.


MAPUMZIKO
Dk 44, Sserunkuma anawatoka mabeki na kumuachia Ibrahim Ajib, lakini anapiga njeeee

Dk 41Mussa Nampaka anapiga shuti kali baada ya kupokea pasi nzuri ya Mgosi lakini linapaa.
Dk 38 Andrew Vicent anaokoa hatari kwenye lango lake na kuzaa kona hata hivyo haina faida
Dk 30, shuti kali la Juuko anapiga shuti kali lakini linapaa juu

Dk 23 Sserunkuma anamtoka Salim Mbonde na kupiga shuti kali, Said Mohammed anaokoa vizuri kabisa.

Dk 21Simba inapata kona safi,
lakiniMkude anapiga shuti juuuuuu
Dk 20, Okwi anapiga shuti kali lakini Okwi anadaka vizuri.


Dk 18, Messi anapiga krosi safi lakini inaokolewa na kuwa kona.

Dk 16, krosi safi, kipa Manyika anafanya kosa lakini Juuko anawahi kuokoa.

Dk 13, Mgosi anapewa pasi nzuri lakini offside

Mtibwa Sugar ndiyo wanaanza kwa mashambulizi mfululizo.

Wanaonekana kufanya mashambulizi ambayo si makali sana. Lakini Simba bado hawajaanza kutia kashkash kwenye lango la Mtibwa Sugar.

REKODI:
Kuanzia mwaka 2010, Simba na Mtibwa Sugar zimekutana mara 9.
katika mechi hizo Simba imeshinda mara 5, sare 2 na Mtibwa Sugar imeshinda 2. 

Simba: 
Peter Manyika, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Mohammed Hussein, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Said Demla, Ramadhani Singano, Dan Sserunkuma, Ibrahimu Ajibu na Emmanuel Okwi.


Mtibwa: 
Saidi Mohammed, Andrew Vicent, David Luhende,  Ally Lundenga, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Nampaka, Muzamiru Yassin, Ame Ally, Mussa Hassan Mgosi na Ally Shomari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic