January 8, 2015


Kikosi cha Polisi Zanzibar kimekuwa cha kwanza kwa timu za visiwani kusonga hadi nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi msimu huu.


Polisi imefanikiwa kutinga nusu fainali kwa kuishinda KCCA ya Uganda kwa mikwaju ya penalti 6-5.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, timu hizo zilimaliza kwa sare ya bila bao dakika 90 na kulazimisha changamoto ya mikwaju ya penalti kuchukua nafasi.

Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali, jana baada ya kuitwanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic