January 22, 2015

 
KIKOSI CHA KWANZA CHA TAIFA STARS MABORESHO...
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kimefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Rwanda maarufu kama Amavubi.


Katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Rwanda ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mzoefu Jean Baptiste Mugiraneza kwa kichwa baada ya mabeki wa Stars kufanya uzembe.

Stars ilisawazisha baadaye kupitia Kelvin Friday Iddi ambaye hata hivyo hakucheza vizuri katika mechi hiyo.

Kiungo Simon Msuva wa Yanga ndiye aliyekuwa msumbufu zaidi kwa mabeki wa Amavubi iliyoongozwa na Haruna Niyonzima.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic