Nahodha Yassine
Chikhaoui ameisaidia timu yake ya Tunisia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya Zambia.
Ushindi huo
umeifanya Tunisia kuongoza Kundi B katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika inayofanyika Equatorial Guinea ikifikisha pointi nne.
Chikhaoui alifunga
bao katika dakika za mwisho kwa kichwa akiunganisha krosi iliyompita kipa
Kennedy Mweene na kupoteza matumaini ya Wazambia.
0 COMMENTS:
Post a Comment