Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi cha Taifa Stars Maboresho kilionyesha soka safi hasa katika kipindi cha pili.
Maboresho imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Rwanda katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza, leo.
Nooij amesema kikosi hicho kimekuwa kiimarika na makosa yanapungua, hivyo ana imani baada ya siku chache zijazo, matunda yataanza kuonekana.
"Naweza kusema makosa yanapungua, sehemu zinakwenda zinaimarika. Hivyo tuamini kuwa kutakuwa na mabadiliko na tuendelee kuwapa moyo vijana," alisema.
Timu hiyo ilishindwa kuonyesha kiwango kizuri katika kipindi cha kwanza, lakini Rwanda wakalazimika kujilinda zaidi kutokana na makali ya Stars Maboresho katika kipindi cha pili.

0 COMMENTS:
Post a Comment