Mshambuliaji wa Yanga
Mrundi, Amissi Tambwe ametamka kuwa, kwa beki ile mbovu anayoijua Simba, basi
wajiandae mara watakapokutana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na Ligi Kuu
Bara.
Mrundi huyo, alijiunga na
timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo lililofungwa Desemba 15, mwaka jana
akitokea Simba baada ya mkataba wake wa miezi sita kusitishwa.
Safu ya ulinzi ya Simba
inaundwa na mabeki wa kati Mganda, Juko Mrushid, Hassani Isihaka na mabeki wa
pembeni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Hassani Kessy, Nassoro Said
‘Chollo’, Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’ na William Lucian ‘Gallas’.
Tambwe amesema kuwa Simba hawana beki wa kuizuia safu yao ya ushambuliaji.
“Nikwambie tu ukweli, kwa
beki ile ya Simba ninayoijua mimi, kazi watakuwa nayo mara tutakapokutana nao
kwa kuanzia huku kwenye Kombe la Mapinduzi na ligi kuu.
“Kwa sababu nikiiangalia
ile safu ya ulinzi na hii safu yetu ya ushambuliaji inayochezwa na Sherman
(Kpah), Msuva (Simon), Mrwanda (Danny) na mimi mwenyewe ni ngumu kushindwa kuwafunga Simba.
“Kiukweli kabisa sisi mbele
tupo vizuri sana kuanzia namba sita kuja juu, hapa ninapokwambia wachezaji wote
tuna hamu ya kukutana na hao Simba wakati wowote ule,”alisema Tambwe.







0 COMMENTS:
Post a Comment