January 6, 2015


Yanga sasa itacheza mechi yake ya robo fainali dhidi ya maafande wa JKU.


Mechi hiyo itapigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Yanga inakutana na JKU baada ya kumaliza vinara wa kundi wakiwa na pointi 9.

Walipata pointi hizo baada ya kushinda mechi tatu kwa mabao tisa, wakiwa hawajafungwa hata moja.

Walikamilisha pointi hizo tisa baada ya leo kuifunga Shaba kwa bao 1-0 katika mechi tamu na ya kuvutia.

Bao la mchezo huo lilifungwa na Mbrazil Andrey Coutinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic